Makamu wa rais wa Tanzania amtembelea Tundu Lissu - Pambazuo

Latest

Business

BANNER 728X90

Wednesday, 29 November 2017

Makamu wa rais wa Tanzania amtembelea Tundu Lissu

Makamu wa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alimtembelea mbunge wa Singida mashariki nchini Tanzania Tundu Lissu ambaye amelazwa katika hospitali ya Nairobi.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, makamu huyo alienda hospitalini humo muda mfupi baada ya kuhudhuria kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta tarehe 28 Novemba.
Bwana Lissu amekuwa akipokea matibabu katika hospitali hiyo tangu mwezi Septemba 7 baada ya kupigwa risasu na watu wasiojulikana katika jaribio la mauaji huko nyumbani kwake mjini Dodoma.
Makamu huyo wa rais ambaye aliandamana na kamishna watanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Chana aliwasili katika hospitali hiyo mwendo wa saa kumi na moja.
Kwa mujibu wa gazeti hilo bi Samia ndio afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Tanzania kumtembelea bwana Lissu miezi mitatu baada ya shambulio.
Bwana Lisuu ambaye pia ni mkuu wa chama cha mawakili nchini Tanzania amekuwa akizozana na serikali ya rais Magufuli na alikamatwa mara sita mwaka huu pekee, akishtumiwa kwa kumtusi kiongozi huyo wa taifa mbali kuharibu usalama wa umma, miongoni mwa mashtaka mengine.
Ndiye kiranja wa bunge wa upinzani na wakili mkuu wa chama cha Chadema.
Alikamatwa mara ya mwisho mnamo mwezi Agosti baada ya kufichua kwamba ndege ilionunuliwa na kampuni ya ndege ya kitaifa Air Tanzania imekamatwa nchini Canada kutokana na deni la shilingi bilioni 83.

No comments:

Post a Comment