Kiungo huyo wa kati wa Uhispania mwenye umri wa miaka 31 alijiunga na Man City kutoka Valencia kwa kitita cha £24m mwaka wa 2010.
Kiungo huyo ameshinda taji la ligi ya Premia mara mbili, kombe la FA na vikombe viwili vya ligi akiwa na City.
Klabu hiyo ya Pep Guardiola imo alama nane mbele kileleni mwa ligi ya Premia baada ya ushindi wa mechi 12, ushindi wao wa hivi karibuni ukiwa siku ya Jumatano dhidi ya Southamton.
Silva, ambaye amesaidia ufungaji wa magoli manane, usaidizi ambao hakuna mchezaji yeyote wa kiwango chake ametimiza, amesema anatarajia kuongeza tuzo zaidi Etihad.
''Najivunia kwa kile nilichojivunia na City kwa misimu saba na nusu hapa pamoja na Pep akiwa meneja. Najihisi tuko katika nafasi nzuri kushinda vikombe msimu huu na kuendelea,'' alisema Silva.
''Mbinu tunayoitumia kucheza soka ni nzuri na ni furaha yangu kuwa miongoni mwao na natarajia kushinda mataji mengi miaka ijayo.
No comments:
Post a Comment